OUR CORE ACTIVITY
Umoja, Ushirikiano na Maendeleo kwa Wanachama wa USHIMWATA na Jamii wa ujumla.
UMOJA WA WANA SHINYANGA, MWANZA, TABORA, GEITA NA SIMIYU
USHIMWATA huwaunganisha wanachama wake kwa kujenga mshikamano, mawasiliano na ushirikiano, huku tukitoa msaada katika nyakati za shida na raha. Tunaendeleza fursa za kiuchumi, kuimarisha ujasiriamali na kuanzisha SACCOS kwa ajili ya kuinua kipato cha wanachama na jamii. Pia tunashirikiana na wadau katika kuhamasisha afya, utunzaji wa mazingira, utamaduni, maadili, amani na maendeleo ya jamii.
Our Functions
“Umoja, Ushirikiano na Maendeleo kwa Wanachama na Jamii.”

USHIRIKIANO
Umoja, Ushirikiano na Maendeleo kwa Wanachama na Jamii.

kIUCHUMI
Kuanzisha na kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi.

USAJIRI SACCOS
Kuanzisha na kusajili SACCOS ya umoja itakayojiendesha.

KUELIMISHA
Wanachama watautumia umoja na wadau wengine katika kutoa elimu.
SHUGHURI ZETU
- Kukuza na kudumisha ushirikiano wa karibu miongoni mwa wanachama wa USHIMWATA.
- Kusaidiana katika matukio mbalimbali ya kijamii yanayohusiana na shida na raha.
- Kuanzisha na kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi kwa faida ya umoja na wanachama
- Kuanzisha na kusajili SACCOS ya umoja itakayojiendesha kwa lengo la kuinua kipato cha wajisiriamali ndani ya umoja na jamii kwa ujumla.
- Wanachama watautumia umoja na wadau wengine katika kutoa elimu ya kutunza na kulinda afya ya jamii, mazingira, utamaduni, mila, desturi, maadili na amani katika jamii.
- Kufanya shughuli nyingine zozote muhimu zinazofanana na zilizoainishwa hapo juu ili kuweza kufikia malengo ya umoja kwa mujibu wa katiba.
