USHIMWATA (Umoja wa Wana Shinyanga, Mwanza, Tabora, Geita na Simiyu) ni umoja unaolenga kuwaunganisha wanachama wake kwa kujenga mawasiliano, mahusiano mazuri na ushirikiano wa karibu kati yao, jamii na taasisi nyingine zenye malengo yanayofanana. Tunajenga umoja kwa kusaidiana katika nyakati za shida na raha, kuimarisha mshikamano wa kijamii na kuendeleza ustawi wa wanachama wetu. Aidha, USHIMWATA huanzisha na kushiriki katika shughuli mbalimbali za kiuchumi zinazolenga kuongeza kipato na fursa za kujikwamua kiuchumi kwa wanachama na jamii kwa ujumla, ikiwemo kuanzisha na kusajili SACCOS ya umoja. Pia, tunashirikiana na wadau mbalimbali kutoa elimu na kuhamasisha jamii kuhusu afya, mazingira, utamaduni, mila na desturi, maadili, amani na maendeleo ya jamii. Kupitia shughuli hizi, USHIMWATA inalenga kuwa jumu
iya imara, yenye mshikamano na inayojali mahitaji na maendeleo ya wanachama wake.
